Saturday, October 27, 2012

MBUNGE WA BUSEGA ATOA CHANGAMOTO KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE BADUGU

Mbunge wa Jimbo la Busega Dr. Titus Kamani ameataka wanafunzi 113 wa Shule ya Sekondari Badugu wajiendeleza zaidi ili wapate elimu ya juu itakayowawezesha kuwa wataalamu wa fani mbalimbali ili kuondoa umasikini na kuleta maendeleo endelevu.

Dr. kamani alitoa kauli hiyo hivi karibuni Katika maafali ya kidato cha nne katika shule hiyo, ambapo pia liwataka wahitimu hao kutoridhika na elimu ya kidato cha nne ambayo alisema kwa sasa ni ya chini mno kutokana na kukuwa kwa utandawazi na tekinolojia duniani.

Kabla ya mahafali hayo mbunge huyo alitembelea mradi wa jengo la maabara la shule ambalo limejengwa na wananchi pamoja na serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 20 ambapo yeye aliahidi kumalizia ujenzi huo kwa fedha kutoak mfuko wa jimbo.

Diwani wa kata hiyo Bw. James Yagaluka alimpongeza mbunge huyo na wazazi wa kata hiyo kwa kujitokeza kujenga sehemu ya jengo hilo la maabara na kuongeza kuwa nyumba mbili za waalimu zinajengwa kwa mpango huo.

Mkuu wa shule hiyo Bw. Isaack Tagaya ameiomba serikali kutakua haraka matatizo yanayoikabili shule hiyo yakiwemo ya ujenzi wa Hosteli ya wasichana ili kuepuka mimba kwa wasichana, uhaba wa maji, upungufu wa walimu na vitabu na ukosefu wa umeme.

Aidha mwalimu Tagaya alieleza mafanikio ya shule hiyo yakiwemo ya kutunza mazingira na usafi wa shule, wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani mbalimbali, shule kuweza kufundisha masomo ya sayansi kwavitendo  na kudumisha michezo ambayo kwa sasa ni ajira na hujenga mwili.

Wanafunzi waliohitimu kidato cha nne shuleni  hapo katika risala yao walisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa, walimu wa masomo ya sayansi na pia ukosefu wa vifaa vya michezo.