Taasisi ya Serengeti Sports Centre ya jimbo la Busega mkoani Simiyu imeandaa mashindano ya mbio za nyika yatakayotambulika kama Serengeti Marathon yanayotaraji kuanza kutimua vumbi mnamo tarehe 11/12/2012.
Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Kayanza Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa mashindano hayo ambayo si washiriki kutoka mkoa wa Simiyu pekee watashiriki, bali pia Serengeti Marathon itashirikisha wafukuza upepo wa mikoa yote kwani tayari taarifa zimefika kwenye vilabu vya vyama vyote nchini vilevile balozi za nchi zote ukanda wa Maziwa Makuu na nchi zote za kimataifa zimepata mialiko, hivyo tutegemee kuona washiriki kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni.
Bofya Play ili upate taarifa kamili,
Bofya Play ili upate taarifa kamili,
Zawadi kwa washindi wa michuano hiyo itakayoshirikisha makundi mawili yaliyotengwa kwa wanaume na wanawake wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea:
Washindi wa kwanza shilingi.....500,000/=
Washindi wa pili shilingi .............400,000/=
Washindi wa tatu shilingi............300,000/=
Washindi wa nne shilingi............200,000/=
Washindi wa tano shilingi...........100,000/=
Nao Washindi wa 6 hadi 10 kwa kila upande (wanawake na wanaume) kuondoka na kifutajasho cha shilingi 20,000/= kila mmoja....