Taasisi ya Serengeti Sports Centre ya jimbo la Busega mkoani Simiyu imeandaa mashindano ya mbio za nyika yatakayotambulika kama Serengeti Marathon yanayotaraji kuanza kutimua vumbi mnamo tarehe 11/12/2012.

Bofya Play ili upate taarifa kamili,
Zawadi kwa washindi wa michuano hiyo itakayoshirikisha makundi mawili yaliyotengwa kwa wanaume na wanawake wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea:
Washindi wa kwanza shilingi.....500,000/=
Washindi wa pili shilingi .............400,000/=
Washindi wa tatu shilingi............300,000/=
Washindi wa nne shilingi............200,000/=
Washindi wa tano shilingi...........100,000/=
Nao Washindi wa 6 hadi 10 kwa kila upande (wanawake na wanaume) kuondoka na kifutajasho cha shilingi 20,000/= kila mmoja....