Saturday, December 1, 2012

MH. WAZIRI MKUU PINDA NDIYE MGENI RASMI SERENGETI MARATHON ITAKAYO TIMUA VUMBI DEC 11/2012


Taasisi ya Serengeti Sports Centre ya jimbo la Busega mkoani Simiyu imeandaa mashindano ya mbio za nyika yatakayotambulika kama Serengeti Marathon yanayotaraji kuanza kutimua vumbi mnamo tarehe 11/12/2012.

Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Kayanza Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa mashindano hayo ambayo si washiriki kutoka mkoa wa Simiyu pekee watashiriki, bali  pia Serengeti Marathon itashirikisha wafukuza upepo wa mikoa yote kwani tayari taarifa zimefika kwenye vilabu vya vyama vyote nchini vilevile balozi za nchi zote ukanda wa Maziwa Makuu na nchi zote za kimataifa zimepata mialiko, hivyo tutegemee kuona washiriki kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni.  

Bofya Play ili upate taarifa kamili, 

 
Zawadi kwa washindi wa michuano hiyo itakayoshirikisha makundi mawili yaliyotengwa kwa wanaume na wanawake wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea:

Washindi wa kwanza shilingi.....500,000/=
Washindi wa pili shilingi .............400,000/=
Washindi wa tatu shilingi............300,000/=
Washindi wa nne shilingi............200,000/=
Washindi wa tano shilingi...........100,000/=
Nao Washindi wa 6 hadi 10 kwa kila upande (wanawake na wanaume)  kuondoka na kifutajasho cha shilingi 20,000/= kila mmoja....

Saturday, October 27, 2012

MBUNGE WA BUSEGA ATOA CHANGAMOTO KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE BADUGU

Mbunge wa Jimbo la Busega Dr. Titus Kamani ameataka wanafunzi 113 wa Shule ya Sekondari Badugu wajiendeleza zaidi ili wapate elimu ya juu itakayowawezesha kuwa wataalamu wa fani mbalimbali ili kuondoa umasikini na kuleta maendeleo endelevu.

Dr. kamani alitoa kauli hiyo hivi karibuni Katika maafali ya kidato cha nne katika shule hiyo, ambapo pia liwataka wahitimu hao kutoridhika na elimu ya kidato cha nne ambayo alisema kwa sasa ni ya chini mno kutokana na kukuwa kwa utandawazi na tekinolojia duniani.

Kabla ya mahafali hayo mbunge huyo alitembelea mradi wa jengo la maabara la shule ambalo limejengwa na wananchi pamoja na serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 20 ambapo yeye aliahidi kumalizia ujenzi huo kwa fedha kutoak mfuko wa jimbo.

Diwani wa kata hiyo Bw. James Yagaluka alimpongeza mbunge huyo na wazazi wa kata hiyo kwa kujitokeza kujenga sehemu ya jengo hilo la maabara na kuongeza kuwa nyumba mbili za waalimu zinajengwa kwa mpango huo.

Mkuu wa shule hiyo Bw. Isaack Tagaya ameiomba serikali kutakua haraka matatizo yanayoikabili shule hiyo yakiwemo ya ujenzi wa Hosteli ya wasichana ili kuepuka mimba kwa wasichana, uhaba wa maji, upungufu wa walimu na vitabu na ukosefu wa umeme.

Aidha mwalimu Tagaya alieleza mafanikio ya shule hiyo yakiwemo ya kutunza mazingira na usafi wa shule, wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani mbalimbali, shule kuweza kufundisha masomo ya sayansi kwavitendo  na kudumisha michezo ambayo kwa sasa ni ajira na hujenga mwili.

Wanafunzi waliohitimu kidato cha nne shuleni  hapo katika risala yao walisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa, walimu wa masomo ya sayansi na pia ukosefu wa vifaa vya michezo. 

Friday, July 6, 2012

KAMATI YA BUNGE YAFANYA ZIARA MWANZA KUTANZUA MGOGORO WA SAMAKI: TUME YABAINI UOZO MWINGI..

Waziri wa mifugo na uvuvi mh. Mathayo David akizungumza na wadau wa samaki Mwanza kulia ni makamu mwenyekiti kamati ya kilimo, mifugo na maji ambaye ni Mbunge wa Vijana DSM Neema Mgaya na wa kwanza kushoto ni wajumbe wa kamati ya kilimo na mifugo Rose Kamili (Mbunge wa viti maalum CHADEMA - Manyara) na mh. Dr. Titus Kamani (Mbunge wa Busega).
Serikali imepiga marufuku uvuvi na uingizwaji wa samaki walio chini ya kiwango kuchakatwa ndani ya viwanda ikiwa ni pamoja na wamikili wake kujihusisha na uvuvi na ununuaji samaki kwenye mialo kanda ya ziwa Victoria.

Tamko hilo limetolewa jana na Waziri wa mifugo na uvuvi Mathayo David Mathayo wakati alipokutana na wavuvi, wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda vya kuchakata minofu ya samaki katika kikao cha kujadili mgogoro uliosababisha wavuvi kugoma na viwanda kutetereka kiuzalishaji.

Wakurugenzi ambao ni wamiliki wa viwanda vya kuchkata samaki jijini Mwanza, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Tanzania Fish Processor (TFP) Ganeshan Vedagir, Amini wa Omega Fish na Peter John wa Nile Perch Fisheries

Kuhusu mgogoro uliodumu takribani mwezi mmoja sasa Waziri David Mathayo, akiwa ameambatana na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Maji na Mifugo, amewashauri wavuvi kuanzisha ushirika wa pamoja utakao wasaidia kutambua bei halali, kudhibiti bei duni na mapungufu yasiyo ya lazima yanayojitokeza.

Mjumbe wa kamati ya kilimo na mifugo Rose Kamili (Mbunge wa viti maalum CHADEMA - Manyara) akiwasilisha jambo kwaajili ya kupata muafaka wa mgogoro baina ya wavuvi na wamiliki wa viwanda Ziwa Victoria, uliosababishwa na wamiliki wa viwanda kushusha bei ya samaki, kulia ni mh. Dr. Titus Kamani (Mbunge wa Busega).
Katika maazimio Kamati hiyo ya bunge imeshauri kuwepo kwa mikataba ya aina moja baina ya wavuvi na wamiliki ambayo itapitiwa na wanasheria wa pande zote mbili chini ya usimamizi wa serikali wakati wa kuandaliwa hatimaye utekelezwaji ili kuepuka migogoro ambayo ni chanzo cha migogoro kupitia dhuruma inayopelekea kuporomoka kwa pato la Taifa.

Mjumbe wa kamati mh. Moshi Selemani Kakoso (Mbunge wa mpanda vijijini) akitoa maelezo ili kupata ufafanuzi.
Suala kubwa lilikuwa ni bei wavuvi wakihitaji bei ipande angalau shilingi 5,000/= kwa kilo moja ya sangara lakini wenye viwanda wamesema kutokana na kushuka kwa ya bei kwenye soko la ulaya hawataweza kupandisha zaidi ya shilingi 3,200/= kwa kilo.


Licha ya kamati hiyo kuwasihi wamiliki wa viwanda kupandisha bei ili kukidhi gharama za mvuvi lakini kutokana na sababu walizoambatanisha wakakomea hapo.

Wavuvi kikaoni.
Tatizo la bei hatimaye mgomo halijawahi kutokea kwenye sekta ya samaki Kanda ya Ziwa lakini kutokana na mapinduzi ya viwanda na kutokuwa na chama cha Ushirika ambacho kingeweza kuwasemea na kunegotiate bei na wanunuzi wa samaki wavuvi imefikia wakati wamekuwa wakinyanyaswa kutokana na kutojua sheria.

Mjumbe wa kamati hiyo toka bungeni mh. Dr. Titus Kamani (Mbunge wa Busega).
Hivyo basi kamati hiyo imetoa mapandekezo kwa wavuvi kuandaa mchakato wa kuanzisha chama cha ushirika ambacho kitakuwa kikiwauzia samaki wenye viwanda na kusimamia bei.

Wakurugenzi wa viwanda mbalimbali Mwanza.
Umuhimu wa kuanzishwa kwa vyama vya Ushirika ulionekana katika Mikoa ya kusini nchini Tanzania ambapo wakulima walikuwa wakitaabika na soko la korosho, manufaa yalionekana mara baada ya serikali kuingilia kati na vyama vya ushirika kufufuliwa, vilivyokuwa havina uwezo wa kukopa vikawezeshwa hatimaye vikaweza kukopesha na hivi sasa vinanunua korosho na kuwauzia wanunuzi wengine kwa minada suala ambalo likivaliwa njuga na wavuvi wa samaki hakika litawapa manufaa.

Meza kuu mkutanoni kutoka kushoto ni wajumbe wa kamati ya kilimo na mifugo Rose Kamili (Mbunge wa viti maalum CHADEMA - Manyara) na mh. Dr. Titus Kamani (Mbunge wa Busega) wakiwa na Waziri wa mifugo na uvuvi mh. Mathayo David.

Suala lingine walilolalamikia wavuvi ni kwamba samaki anapo fikishwa kiwandani na kutajwa kuwa ni reject harudishwi na kiwanda hivyo kamati hiyo imetamka kuwa kama samaki ni reject basi arudishwe kwa mvuvi badala ya viwanda kuchukuwa reject hao.

Mkurugenzi wa Monarch Hotel Mwanza Osward m. Mwizarubi akizungumza na Waziri wa mifugo na uvuvi mh. Mathayo David mara baada ya kumalizika kwa majumuisho ya kutanzua mgogoro baina ya wavuvi na wamiliki wa viwanda vya samaki yaliyofanyika hotelini hapo.
Wavuvi hao wamelalamika kitendo cha wamiliki wa viwanda kutowaruhusu kuingia viwandani kushuhudia uzito na kupitia hilo kamati imesema wazi kuwa huo ni wizi hivyo imeagiza wanunuzi na wenye viwanda kuwaruhusu wavuvi kuingia viwandani kushuhudia upimwaji na kujua uzito halali wa mali waliyouza ili kupata haki zao.

Thursday, June 28, 2012

MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA SERIKALI ZA MITAA 2012

 
Sherehe za maadhimisho ya siku ya Serikali za mitaa zinafanyika jijini Mwanza, sherehe zikifanyika kwa ushirikiano wa jumuiya za serikali za mitaa Alat na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI.

Maadhimisho hayo yanafanyika sasa katika uwanja wa CCM Kirumba tangu tarehe 24 juni hadi tarehe 1 july 2012 na kuhusisha shughuli mbalimbali mathalani Kongamano la kuboresha ubia baina ya sekta za Umma na Binafsi.

Wananchi wakiwa katika banda mojawapo uwanjani humo wakionja ladha ya mvinyo mmoja wapo unaotengenezwa na viwanda vidogo hapa nchini.

Kauli mbiu kwa maadhimisho haya kwa mwaka huu ni 'Shiriki sensa ya watu toa maoni kuhusu katiba mpya kuharakisha ugatuaji wa madaraka kwa wananchi kwa maendeleo yao'

Ufugaji bora nao unahusishwa kwenye maonyesho haya.

Wananchi kwenye baadhi ya mabanda.

Ramani picha ikionesha mpango wa jinsi jiji la Mwanza litakavyokuwa kufikia mwaka 2025.

Sunday, March 11, 2012

SAFARI YA CCM KUVISAKA VITI VYAKE YAANZA KWA KISHINDO MWANZA.

"Nichagulieni jembe hili linalofiti viganja vyangu" Spika wa zamani wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samweli Sita akimnadi kwa wananchi bw. Jack Masamaki kwa wananchi wa Kirumba Mwanza kwaajili ya kinyang'anyiro cha kiti cha udiwani kata hiyo.
Mpiganaji Jack 'Masamaki' kupitia tiketi ya CCM, alimwaga sera kwa wananchi wa kata yake kisha akapata nafasi ya kuomba kura.
Sehemu ya umati uliofurika kwenye uwanja wa Magomeni Kirumba katika mkutano wa hadhara wa kwanza wa kumnadi mgombea wa kiti cha udiwani kata ya Kirumba Mwanza, uchaguzi huu unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani ya kata hiyo marehemu Novatus Manoko.
"Mexico wamemudu sana ujenzi wa barabara sehemu za milima uko mkakati kuwawezesha madiwani wa Mwanza kufanya ziara wakaone ni jinsi gani wataboresha barabara sehemu za milima, wajifunze njia nyepesi za ujenzi wa barabara katika maeneo yote yanayopitika kwa tabu hivyo ndugu yangu Magufuli ajiandae kwani tunakwenda kushikamana" alisema Mh Samweli Sita
'Kubaliko' kwa vijana.
Mh. Sita akishuka jukwaani na Jack Masamaki kuanza maandamano mara baada ya mkutano kumalizika.
Mh Sita -" Mie kifaa' Umeona mambo yangu jukwaani....???" Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza- Umetisha mheshimiwa...!!!
Kutoka kushoto meneja wa uwanja wa CCM Kirumba John Tegete, Mgombea udiwani Jack Masamaki na Mh. Sita.
Safari ikaanza kupita mitaani ambapo kituo cha mwisho ilikuwa ni ofisi za CCM kata ya Kirumba.
Akinamama walifunga vibwebwe kuhakikisha wanamuunga mkono mwana wao wa nyumbani kufanikisha adhma yake iliyo na nia njema kwa wakazi wa kata ya Kirumba.
Ngoma inogile.......
Salaaamu kwa wadau wa ukweli mitaa ya Kirumba Polisi.........
Msafara ulikatisha sokoni kwa mbwembwe ukitoa salamu kwa wapiga kura...