Sherehe za maadhimisho ya siku ya
Serikali za mitaa zinafanyika jijini Mwanza, sherehe zikifanyika kwa ushirikiano
wa jumuiya za serikali za mitaa Alat na Ofisi ya Waziri Mkuu
TAMISEMI.
Maadhimisho hayo yanafanyika
sasa katika uwanja wa CCM Kirumba tangu tarehe 24 juni hadi tarehe 1 july 2012
na kuhusisha shughuli mbalimbali mathalani Kongamano la kuboresha ubia baina ya
sekta za Umma na Binafsi.
Wananchi wakiwa katika banda mojawapo
uwanjani humo wakionja ladha ya mvinyo mmoja wapo unaotengenezwa na viwanda
vidogo hapa nchini.
Kauli mbiu kwa maadhimisho haya kwa
mwaka huu ni 'Shiriki sensa ya watu toa maoni kuhusu katiba mpya kuharakisha
ugatuaji wa madaraka kwa wananchi kwa maendeleo yao'
Ufugaji bora nao unahusishwa kwenye
maonyesho haya.
Wananchi kwenye baadhi ya
mabanda.
Ramani picha ikionesha mpango wa jinsi
jiji la Mwanza litakavyokuwa kufikia mwaka 2025.
No comments:
Post a Comment