Tuesday, January 24, 2012

MBUNGE WA BUSEGA ALIPOTEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA SISTERS OF HOPE

Katika kuwatia moyo na kuhakikisha watoto hawa wanaishi japo katika halistahiki mbunge wa Busega Dr. Kamani alidhuru kituo cha Hope sisters kilichopo jimboni kwake kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali na kujionea changamoto mbalimbali zilizopo kituoni hapo.

                          Mh mbunge alishiriki hata kwenye michezo yao na simulizi za utii. 
Watoto hawa hucheza kama watoto wengine hasa pale wanapopatiwa huduma muhimu pichani wakiwa na Sister mlezi wa kituo cha Sisters of Hope anayewakarimu kama mama wa watoo hawa kweli inatia moyo.
Ni watoto wasikivu wenye utii, wanaopendana hapa walikuwa wakisikiliza neno toka kwa mlezi wao mh. mbunge aliye watembelea .

Monday, January 9, 2012

MBUNGE WA BUSEGA Dr. KAMANI AFANYA UKAGUZI WA MABWAWA YA SAMAKI YA WAJASILAMALI JIMBONI KWAKE.

Mbunge wa Jimbo la Busega mkoa wa Mwanza Mh. Dr.Titus Kamani, Mlengeya akikaguwa moja ya mabwawa ya mradi wa kufuga samaki kijiji cha Badugu.

Mradi wa kuhamasisha wananchi kufuga zao la samaki unakuja ukiwa na lengo la kutimiza Ilani ya Serikali ya Tanzania kuwawezesha wananchi wa vijiji nchini kiuchumi hasa linapokuja suala la ujasiliamali nalo zao hilo likiwa ni moja ya mazao yenye kipato kikubwa.

Lengo lingine lililozingatiwa kuhamasisha ufugaji wa samaki kupitia mabwawa ya kaya kwa kaya ni kuendana na kasi ya mahitaji.

Soko la samaki limekuwa kubwa ndani na nje ya nchi nao samaki wenye viwango kwa ziwa victoria wanazidi kupungua siku baada ya siku kutokana na uvuvi haramu ulioshamiri kwenye baadhi ya maeneo na kingo za mwambao wa ziwa Victoria.

Hivyo basi kupitia miradi kama hii kuna uhakika kwa wananchi kupata samaki wakubwa wenye viwango vinavyohitajika kwenye soko hasa la kimataifa.


Hili ni moja kati ya mabwawa makubwa ya kisasa yaliyojengwa jimboni Busega kwaajili ya ufugaji samaki, likiwa na uwezo wa kufuga samaki tani kadhaa liko mbioni kukamilika.

Tayari wajasilia mali mbalimbali kutoka vijiji vinne vilivyopo kando kando ya ziwa Victoria, jimbo la Busega kama vile Lamadi, Manala, Kalmela na Shimanilwe wameitikia wito kujiunga kwenye uwekezaji huo.

Saturday, January 7, 2012

KARIBU KATIKA UWEKEZAJI MPYA WA UTALII NCHINI

Sun set eneo tulivu.

Kutoka mbali moja ya hotel itakuelekeza macho yako kuona eneo hili la mbuga ya hifadhi...

Mbuni sawia kwenye hifadhi.

Mh. Mbunge Dk. Kamani wa jimbo la Busega eneo lililo na hifadhi hii ya Taifa.

Kila mmoja ana jukumu la kutangaza Utalii wa ndani wa nchi hii.


Makaribisho ya asubuhi na mapema.

Si wageni tu bali hata wenyeji hudhuru vivutio vya utalii jimbo la Busega linalopakana na mbuga mashuhuri ya Serengeti.

Swala.

Huwa nawachanganya majina wanyama hawa .... wengine huwaita Tumbili, wengine Nyani, wengine Kima na majina mengiiii.....

Sekta nzima ya Utalii jimbo la Busega imelenga.1.Kuunganisha waendesha biashara ya utalii katika mkoa wa Mwanza ili kuweza kulitangaza eneo la ukanda huu kwa pamoja.
2.Kuongeza utangazaji wa utalii katika mwambao wa ziwa Victoria ili kuongeza biashara ya utalii katika eneo lililopo jimboni.
3.Kuvutia uwekezaji wa mahoteli katika mwambao wa ziwa Victoria na pembeni mwa vilima jimboni, na kuhamasisha michezo ya majina na meli za starehe.
4.Kubainisha mambo ya kale na shughuli za kiutamaduni zilizopo jimboni zinazofaa kutumika kama kivutio cha utalii.
5.Kufundisha wananchi ili waweze kushiriki katika biashara ya utalii.

Thursday, January 5, 2012

UFUGAJI NYUKI NA UTUNZAJI MAZINGIRA

Ufugaji nyuki
1. Kuleta waelimishaji wa ufugaji nyuki toka TAWIRI/SIDO/Idara ya Misitu na Nyuki.
2. Kuanzisha vikundi vya ufugaji nyuki Badugu, Nyaluhande, Ngasamo, Kiloleli, Mwamanyili, Kabita, Shigala, Igalukilo, Malili, Mkula na Kalemela.
3. Kujifunza na kusindika mazao ya nyuki.
4. Kubaini na kuvutia masoko ya mazao ya nyuki (mf. Mohamed Enterprises kwa ajili ya nta).

Mazingira
1. Kuhamasisha upandaji miti kama zao la biashara – kwa familia na taasisi (kushirikiana na Tanzania Tree Seed Agency – TTSA, SUA, Chuo cha Olmotonyi na NGOs mf. Acord, Lake Victoria Environment Management Programme – LVEMP).
2. Kuanzisha miradi ya vitalu vya miti kibiashara – kwa taasisi na watu binafsi kwa kata na vijiji.
3. Kuhamasisha na kuwawezesha vijana waliomaliza mafunzo kwenye vituo vya ufundi (vocational training) kuanzisha miradi ya ufundi ya kuongeza thamani ya mazao ya miti.

Monday, January 2, 2012

UVUVI


Uvuvi
1. Kutoa elimu ya uvuvi kwa maeneo yote ya mwambao wa ziwaVictoria.
2. Kuanzisha mtandao wa wavuvi.
3. Kuanzisha vyama vya kuweka na kukopa vya wavuvi (SACCOS).
4. Kuendeleza bandari muhimu katika jimbo – Kiloleli, Mwamanyili, Kabita (Nyamikoma) na Kalemela (Lamadi, Kalemela).
5. Kuhamasisha na kuendeleza ufugaji wa samaki. (Ushauri utapatikana kwa Dr Yohana Budeba/TAFIRI).
6. Kuanzisha utaalamu wa kuongeza thamani ya mazao ya samaki ikiwemo kukausha na kufunga (packaging) kwa kusafirisha nje ya nchi mf. Congo, Burundi na Kenya.

MALENGO YA SEKTA KILIMO NA UFUGAJI JIMBO LA BUSEGA


Kilimo na Ufugaji
1. Kufanya Tathimini ya udongo katika jimbo ili kubaini mazao stahili kwa maeneo mbalimbali (Refer Agricultural Reseach Institute (ARI) – Ukiriguru. Dr.Kileo)


2. Kuboresha mbegu za mifugo (ng’ombe, mbuzi na kondoo) kwa kuanzisha kituo cha uhamasishaji (artificial insemination) Nyashimo; na kituo cha madume bora Igalukiro.


3. Kufundisha na kuhamasisha matumizi ya elimu ya malisho ya mifugo kwa wafugaji na kuanzisha mashamba ya mbegu za malisho kwenye vituo vya mafunzo Jimboni.


4. Kuanzisha, kuboresha na kulinda maeneo ya malisho ya mifugo zikiwamo ‘’ngitiri” na kutumia mipango ya matumizi bora ya ardhi vijijini (village land use plans).


5. Kuhamasisha ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa wanawake na vijana na kutengeneza mtandao wa soko. Kutumia uzoefu wa wanawake wa mutukula – kagera (Refer TASAF/Mwamanga/Dr. Mwamuhehe – VIC Iringa). Walianza na kuku 1,000 na katika kipindi cha mienzi9 walikua tayari na mil.97 benki, mwaka mmoja wakawa na mil.120.


6. Kuanzisha soko la kimataifa la mbuzi mwasamba na maonyasho ya mifugo bora.


7. Kuimarisha vikundi vya wakulima.


8. Kuhamasisha shughuli ya unenepeshaji ng’ombe na mbuzi kwa ajili ya soko la kimataifa mf. Comoro, Falme za kiarabu, Kongo, Burundi, Kenya na Sudan.


9. Kuanzisha ukulima wa mazao mapya mf. Alzeti, dengu, choroko, mbaazi nk.


10. Kuhamasisha matumizi ya zana za kisasa za kilimo(agromechanization) kwa kuongeza matumizi ya matrekta, power tillers na plau (Refer Binti Nanai – Mrs.Kaali, Wizara ya kilimo, ARI-Uyole, SUA-Animal science Department, Prof.Abud).


11. Kufufua kituo cha agromechanization Malili/Igalukilo. (kushirikiana na Roman Catholic – jimbo la Shinyanga).


12. Kuhamasisha matumizi ya pembejeo za kilimo kama vile mbolea na mbegu bora kwa kutoa mafunzo kwa wakulima na kuanzisha maduka ya pembejeo kwa kila kata.


13. Kuanzisha vituo vya mafunzo ya kilimo Nyaluhande na Malili.


14. Kuanzisha ziara za mafunzo za wakulima na viongozi stahili kwenye vyuo vya kilimo, taasisi za utafiti za kilimo, maonyesho ya kilimo nk.


15. Kuanzisha mtandao wa mabwana shamba na mabwana mifugo jimboni ili kubadilishana mawazo na kuongeza hamasa ya kazi.


16. Kuanzisha mfumo wa mafunzo endelevu (continuing education/retraining) wa maafisa ugani wa kilimo na mifugo ili kuingiza maarifa mapya ya kilimo na ufugaji jimboni (Refer FAO, UNDP, ASDP)


17. Kuhamasisha na kuanzisha kilimo cha umwagiliaji kwenye Bonde la mto Duma na Bonde la ziwa Victoria. (kutumia uzoefu wa Miradi ya Arumeru, Lushoto, wizara ya kilimo, chuo cha kilimo na kiyuo cha utafiti wa kilimo Ukiriguru na kituo cha umwagiliaji kanda ya ziwa-Nyakato.


18. Kuanzisha vikosi vya kutengeneza miundombinu ya umwagiliaji kama vile mabwawa (charco dams) kwenye mito na mabonde yote jimboni. Kata mbili zitaanziwa kama eneo la mfano (pilot project). Vitendea kazi muhimu ni D4 moja na tipper mbili kwa kila kata. Kata za mwanzo ni Kiloleli na Mkula.


19. Kuanzisha namna ya kuongeza thamani ya mazao kabla ya kuuza mf. Biltong, kuyapima na kupaki kwenye mifuko nk.


20. Kuanzisha kitengo cha masoko katika ofisi ya mbunge ili kutafuta masoko na bei bora za mazao kwa kushirikiana na mkurugenzi wa maendeleo wa wilaya. Mpango huu wa kuimarisha kilimo na mifugo utajengwa katika misingi ya kupambana na njaa na kujanisha Busega kwa kuunga mkono mpango wa Taifa wa Kilimo Kwanza.

Sunday, January 1, 2012

MIPANGO YA KISEKTA


SEKTA YA UCHUMI
Fedha na Biashara
1. Kuanzisha na kuimarisha vikundi vya uzalishaji /SACCOS/ VICOBA kwa kuwaongezea mitaji na elimu ya biashara (kutumia uzoefu wataalam wa maendeleo ya jamii na Ushirika, Plan International – Daniel Kalimbiya)

2. Kuunganisha SACCOS zote ili kuanzisha Benki ya Wananchi wa Busega. Dhamira ni kuyakarabati na kuyatumia majengo yaliyokuwa ya Victoria Federation yaliyopo Mwagulanja. Benki ya Wanawake inaweza kuwa hatua nyingine.

3. Kuanzisha Benki za Mazao – kutumia uzoefu wa Mikoa ya Nyanda za juu kusini (Mbeya, Iringa na Ruvuma) kwa kufanya ziara huko ya wahusika muhimu.

4. Kutoa elimu ya ujasirimali, mikopo na utunzaji wa mahesabu. Wataalam watapatikana kwa kutumia Baraza la Taifa la Uwekezaji Kiuchumi, UDEC nk.

5. Kuunganisha wafanyakazi (business matching) kikanda (regionally) na kimataifa (Internationally) kwa kutumia TCCIA na Kituo cha Uwekezaji (TIC).

6. Kuhamasisha na kuvutia ufunguaji wa biashara kubwa na uwekezaji katika maeneo ya jimbo.

7. Kuhamasisha ujenzi wa viwanja vya kusindika mazao ya kilimo na mifugo mf. Nafaka nk.

8. Kuhamasisha na kuwezesha ushiriki katika maonyesho ya biashara kitaifa na kimataifa – Dar es salaam, Mwanza, Nairobi nk.

9. Kujenga kituo cha mabasi Lamadi/Nyashima ili kuongeza chanzo cha mapato kwa mfuko wa maendeleo ya jimbo na Halmashauri ya Wilaya.