Mbunge wa Jimbo la Busega mkoa wa Mwanza Mh. Dr.Titus Kamani, Mlengeya akikaguwa moja ya mabwawa ya mradi wa kufuga samaki kijiji cha Badugu.
Mradi wa kuhamasisha wananchi kufuga zao la samaki unakuja ukiwa na lengo la kutimiza Ilani ya Serikali ya Tanzania kuwawezesha wananchi wa vijiji nchini kiuchumi hasa linapokuja suala la ujasiliamali nalo zao hilo likiwa ni moja ya mazao yenye kipato kikubwa.
Lengo lingine lililozingatiwa kuhamasisha ufugaji wa samaki kupitia mabwawa ya kaya kwa kaya ni kuendana na kasi ya mahitaji.
Soko la samaki limekuwa kubwa ndani na nje ya nchi nao samaki wenye viwango kwa ziwa victoria wanazidi kupungua siku baada ya siku kutokana na uvuvi haramu ulioshamiri kwenye baadhi ya maeneo na kingo za mwambao wa ziwa Victoria.
Hivyo basi kupitia miradi kama hii kuna uhakika kwa wananchi kupata samaki wakubwa wenye viwango vinavyohitajika kwenye soko hasa la kimataifa.
Hili ni moja kati ya mabwawa makubwa ya kisasa yaliyojengwa jimboni Busega kwaajili ya ufugaji samaki, likiwa na uwezo wa kufuga samaki tani kadhaa liko mbioni kukamilika.
Tayari wajasilia mali mbalimbali kutoka vijiji vinne vilivyopo kando kando ya ziwa Victoria, jimbo la Busega kama vile Lamadi, Manala, Kalmela na Shimanilwe wameitikia wito kujiunga kwenye uwekezaji huo.
No comments:
Post a Comment