Sunday, January 1, 2012

MIPANGO YA KISEKTA


SEKTA YA UCHUMI
Fedha na Biashara
1. Kuanzisha na kuimarisha vikundi vya uzalishaji /SACCOS/ VICOBA kwa kuwaongezea mitaji na elimu ya biashara (kutumia uzoefu wataalam wa maendeleo ya jamii na Ushirika, Plan International – Daniel Kalimbiya)

2. Kuunganisha SACCOS zote ili kuanzisha Benki ya Wananchi wa Busega. Dhamira ni kuyakarabati na kuyatumia majengo yaliyokuwa ya Victoria Federation yaliyopo Mwagulanja. Benki ya Wanawake inaweza kuwa hatua nyingine.

3. Kuanzisha Benki za Mazao – kutumia uzoefu wa Mikoa ya Nyanda za juu kusini (Mbeya, Iringa na Ruvuma) kwa kufanya ziara huko ya wahusika muhimu.

4. Kutoa elimu ya ujasirimali, mikopo na utunzaji wa mahesabu. Wataalam watapatikana kwa kutumia Baraza la Taifa la Uwekezaji Kiuchumi, UDEC nk.

5. Kuunganisha wafanyakazi (business matching) kikanda (regionally) na kimataifa (Internationally) kwa kutumia TCCIA na Kituo cha Uwekezaji (TIC).

6. Kuhamasisha na kuvutia ufunguaji wa biashara kubwa na uwekezaji katika maeneo ya jimbo.

7. Kuhamasisha ujenzi wa viwanja vya kusindika mazao ya kilimo na mifugo mf. Nafaka nk.

8. Kuhamasisha na kuwezesha ushiriki katika maonyesho ya biashara kitaifa na kimataifa – Dar es salaam, Mwanza, Nairobi nk.

9. Kujenga kituo cha mabasi Lamadi/Nyashima ili kuongeza chanzo cha mapato kwa mfuko wa maendeleo ya jimbo na Halmashauri ya Wilaya.

No comments:

Post a Comment