Monday, January 2, 2012

MALENGO YA SEKTA KILIMO NA UFUGAJI JIMBO LA BUSEGA


Kilimo na Ufugaji
1. Kufanya Tathimini ya udongo katika jimbo ili kubaini mazao stahili kwa maeneo mbalimbali (Refer Agricultural Reseach Institute (ARI) – Ukiriguru. Dr.Kileo)


2. Kuboresha mbegu za mifugo (ng’ombe, mbuzi na kondoo) kwa kuanzisha kituo cha uhamasishaji (artificial insemination) Nyashimo; na kituo cha madume bora Igalukiro.


3. Kufundisha na kuhamasisha matumizi ya elimu ya malisho ya mifugo kwa wafugaji na kuanzisha mashamba ya mbegu za malisho kwenye vituo vya mafunzo Jimboni.


4. Kuanzisha, kuboresha na kulinda maeneo ya malisho ya mifugo zikiwamo ‘’ngitiri” na kutumia mipango ya matumizi bora ya ardhi vijijini (village land use plans).


5. Kuhamasisha ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa wanawake na vijana na kutengeneza mtandao wa soko. Kutumia uzoefu wa wanawake wa mutukula – kagera (Refer TASAF/Mwamanga/Dr. Mwamuhehe – VIC Iringa). Walianza na kuku 1,000 na katika kipindi cha mienzi9 walikua tayari na mil.97 benki, mwaka mmoja wakawa na mil.120.


6. Kuanzisha soko la kimataifa la mbuzi mwasamba na maonyasho ya mifugo bora.


7. Kuimarisha vikundi vya wakulima.


8. Kuhamasisha shughuli ya unenepeshaji ng’ombe na mbuzi kwa ajili ya soko la kimataifa mf. Comoro, Falme za kiarabu, Kongo, Burundi, Kenya na Sudan.


9. Kuanzisha ukulima wa mazao mapya mf. Alzeti, dengu, choroko, mbaazi nk.


10. Kuhamasisha matumizi ya zana za kisasa za kilimo(agromechanization) kwa kuongeza matumizi ya matrekta, power tillers na plau (Refer Binti Nanai – Mrs.Kaali, Wizara ya kilimo, ARI-Uyole, SUA-Animal science Department, Prof.Abud).


11. Kufufua kituo cha agromechanization Malili/Igalukilo. (kushirikiana na Roman Catholic – jimbo la Shinyanga).


12. Kuhamasisha matumizi ya pembejeo za kilimo kama vile mbolea na mbegu bora kwa kutoa mafunzo kwa wakulima na kuanzisha maduka ya pembejeo kwa kila kata.


13. Kuanzisha vituo vya mafunzo ya kilimo Nyaluhande na Malili.


14. Kuanzisha ziara za mafunzo za wakulima na viongozi stahili kwenye vyuo vya kilimo, taasisi za utafiti za kilimo, maonyesho ya kilimo nk.


15. Kuanzisha mtandao wa mabwana shamba na mabwana mifugo jimboni ili kubadilishana mawazo na kuongeza hamasa ya kazi.


16. Kuanzisha mfumo wa mafunzo endelevu (continuing education/retraining) wa maafisa ugani wa kilimo na mifugo ili kuingiza maarifa mapya ya kilimo na ufugaji jimboni (Refer FAO, UNDP, ASDP)


17. Kuhamasisha na kuanzisha kilimo cha umwagiliaji kwenye Bonde la mto Duma na Bonde la ziwa Victoria. (kutumia uzoefu wa Miradi ya Arumeru, Lushoto, wizara ya kilimo, chuo cha kilimo na kiyuo cha utafiti wa kilimo Ukiriguru na kituo cha umwagiliaji kanda ya ziwa-Nyakato.


18. Kuanzisha vikosi vya kutengeneza miundombinu ya umwagiliaji kama vile mabwawa (charco dams) kwenye mito na mabonde yote jimboni. Kata mbili zitaanziwa kama eneo la mfano (pilot project). Vitendea kazi muhimu ni D4 moja na tipper mbili kwa kila kata. Kata za mwanzo ni Kiloleli na Mkula.


19. Kuanzisha namna ya kuongeza thamani ya mazao kabla ya kuuza mf. Biltong, kuyapima na kupaki kwenye mifuko nk.


20. Kuanzisha kitengo cha masoko katika ofisi ya mbunge ili kutafuta masoko na bei bora za mazao kwa kushirikiana na mkurugenzi wa maendeleo wa wilaya. Mpango huu wa kuimarisha kilimo na mifugo utajengwa katika misingi ya kupambana na njaa na kujanisha Busega kwa kuunga mkono mpango wa Taifa wa Kilimo Kwanza.

No comments:

Post a Comment